Hali ya kibinadam ni janga asema Malek

Aliyekuwa mmoja wa waangalizi wa jumuiya ya nchi za Kiarabu nchini Syria, ametaja harakati za waangalizi hao kama mzaha na kuilezea hali nchini humo kama janga la kibinadam.

Anwar Malek, ambaye ni raia wa Algeria, ameiambia televisheni ya Al-Jazeera kuwa alijihuzulu kutoka ujumbe huo wa waangalizi kutokana na yale aliyoshuhudia nchini Syria.

Amesema kuwa ujumbe wa waangalizi hao unasambaratika na wanajeshi watiifu kwa rais Bashar al-Assad wanatekeleza uhalifu wa kivita kwa kuwapiga risasi raia ovyo ovyo,kuwateka nyara na kuwanyanyasa.