Wakosoaji waachiliwa huru Burma

Wakosoaji muhimu wa kisiasa nchini Burma wameachiliwa kutoka gerezani - katika matukio ya hivi karibuni ya msamaha kwa wafungwa.

Walioachiliwa ni pamoja na wakongwe wa mwaka 1988 wa vuguvugu la migomo, watawa waliohusika na maandamano ya mwaka 2007 na wanaharakati wa kikabila.

Maarufu zaidi katika wafungwa hao ni Min Ko Naing, kiongozi wa jaribio lililoshindikana la mwaka 1988.

Kituo cha taifa cha TV kimetangaza wafungwa 651 wataachiliwa katika mpango wa msamaha wa rais, lakini hakikusema wangapi watakuwa wafungwa wa kisiasa.

Burma imekabiliwa na wito kutoka kwa jamii ya kimataifa ya kuwaachilia huru wakosoaji zaidi.