Goodluck ataka Boko Haram kujitambulisha

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amewataka viongozi wa kundi la wapiganaji wa kiislam la Boko Haram, kujitokeza hadharani na kutangaza wanachotaka kama njia ya kufungua majadiliano na serikali.

Amesema makabiliano ya kijeshi pekee hayatasaidia kumaliza mashambulio ya kigaidi ambayo yanatishia usalama wa nchi hiyo.

Rais huyo amesema ikiwa hawatajitambulisha basi hakuwezi kufanyika majadaliano yoyote na kundi hilo.

Tamko hilo la Goodluck linakuja baada ya kiongozi wa Boko Haram kukanusha kuwa walihusika na mashambilizi ya hivi karibuni katika mji wa Kano uliosababisha vifo vya watu 185.