Matokeo ya ubunge yatangazwa DRC

Matokeo ya uchaguzi wa viti vya bunge katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yametangazwa usiku wa kuamkia leo. Chama tawala chake Rais Joseph Kabila cha PPRD kimepata viti hamsini na nane na washirika wake wamepata ushindi maradufu ya muungano wa vyama vya upinzani uliongozwa na Etienne Tshisekedi.

Uchaguzi huo ulifanyika Novemba mwaka jana sawa na uchaguzi wa urais, ambapo Rais Joseph Kabila aliibuka mshindi. Ulikumbwa na madai ya wizi wa kura na dosari katika mfumo wa uchaguzi.

Tume ya uchaguzi imewashauri wanaodhani waliibiwa kura zao kuwasilisha kesi mahakamani. Na bila shaka wengi wanatarajiwa kufanya hivyo kutokana na dosari zilizokumba uchaguzi huo na pia shughuli ya kuzihesabu.