Aung Sang Suu Kyi awa mgombea rasmi

Kiongozi wa upinzani nchini Burma, Aung San Suu Kyi, kwa mara ya kwanza anasafiri nje ya mji wake wa nyumbani akiwa mgombea rasmi katika uchaguzi ujao.

Bi Suu Kyi anazuru eneo la delta ya Irrawaddy lililokuwa limeathiriwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kimbunga Nargis mwaka 2008.

Ni miaka 20 sasa tangu afike katika eneo hilo. Wakati huo huo Marekani imeondoa baadhi ya vikwazo ambapo kwa sasa taasisi za fedha za kimataifa zitaweza kutoa msaada kwa Burma.

Bii Suu Kyi amesema kampeini za uchaguzi wa chama chake zitaelekeza katika utawala wa sheria , maendeleo na maridhiano ya kitaifa. Amewaomba wapiga kura kukichagua chama chake cha NLD kuongoza nchi ya Burma.