Raia wa Marekani ni mshirika wa Al Qaeda

Raia wa Marekani mzaliwa wa Pakistan ambaye anajishughulisha na kazi ya kuendesha taxi amekiri mbele ya mahakama moja mjini Chicago, Marekani kwa kutoa fedha kwa mtu mwenye uhusiano na kikundi cha wapiganaji wa Al-Qaeda.

Raja Lahrasib Khan, ambaye ni raia wa Marekani, amekiri kuwa alimpa mamia kadha ya dola za Kimarekani Ilyas Kashmiri, mpiganaji wa Pakistan mwenye kutuhumiwa kuwa na uhusiano na Al-Qaeda na vikundi vingine vyenye makao yao nchini Pakistan.

Khan amekiri kukutana na Kashmiri mara mbili.

Kwa sasa anabakia mahabusu hadi mwezi Mei atakapohukumiwa.