watu 9 wauawa Mogadishu

Polisi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wamasema watu 9 wakufua kufuatia shambulio la bomu la kujitoa mhanga lilolotokea karibu na Ikulu ya rais na hoteli ya Muna.

Idara ya polisi inasema mlipuko huo ulitokea karibu sana na hoteli hiyo ya Muna, eneo ambalo hutumia sana na wanasiasa na watumishi wa serikali kwa mikutano yao.

Wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab wameiambia BBC kuwa wao ndio waliotekeleza shambulio hilo.

Kundi hilo limetuhumiwa kufanya mashambulio ya mara kwa mara mjini Mogadishu, licha ya kuwa wametimuliwa kutoka mji huo wa wanajeshi wa serikali ya mpito TFG kwa ushirikiano na wanajeshi wa kutunza amani wa Muungano wa Afrika.