Rais wa Syria atoa ahadi

Rais wa Syria, Bashar al-Assad, ametoa ahadi mpya ya kumaliza ghasia nchini mwake, kuzungumza na makundi ya upinzani na kuleta mabadiliko.

Alitoa ahadi hiyo kwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov.

Hata hivyo makundi ya upinzani, ambayo yamekuwa yakishambuliwa kwa siku nne mfululizo katika ngome yao ya Homs, yamemlaumu Rais Assad kwa kutoa ahadi za uongo.

Bwana Lavrov alisema kuwa anaamini kwamba Rais Assad anaelewa umuhimu wa kuchukua hatua ya dharura.

Lakini hata hivyo makundi ya upinzani yalisema hayaamini anayosema.

Balozi wa Urushi katika Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin, alisema kuwa anafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa anazuia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo ambavyo vinaweza kuvuruga amani katika eneo hilo lote.