Fabio Capello ajiuzulu

Meneja wa timu ya Uingereza, Fabio Capello, amejiuzulu.

Mtaliano huyo amekuwa katika mzozo na shirikisho la kandanda la Uingereza baada ya shirikisho hilo kumwondoa John Terry kama nadhodha wa timu yake bila yeye kushirikishwa katika uamuzi huo.

Capello ameshutumu uamuzi wa shirikisho hilo hadharani.

Terry anakabiliwa na shutuma ya kumtukana mchezaji mwenzake kwa lugha ya ubaguzi wa rangi.

Capello amejiondoa miezi michache kabla ya Uingereza kushindana katika kombe la mataifa Bingwa Barani Ulaya.