Mwanajeshi mkuu mahakamani Guinea

Upande wa Mashtaka nchini Guinea umemfikisha mahakamani afisa mmoja wa cheo cha juu wa jeshi kwa mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya waandamanaji waliokuwa wakipinga Serikali ya kijeshi ya 2009.

Mshtakiwa, Kanali Moussa Tiegboro Cama, ndiye afisa wa cheo cha juu zaidi nchini humo kushtakiwa kwa makosa hayo.

Zaidi ya watu 150 waliuawa wakati wanajeshi waliposhambulia mkutano wa waandamanaji katika uga mmoja mjini Conakry, na zaidi ya wanawake 100 walibakwa katika tukio hilo.

Utawala wa kijeshi ulimalizika wakati Rais Alpha Conde alipochaguliwa.