Marekani:wanawake kuruhusiwa vitani

Jeshi la marekani limetangaza mipango mipya ya kuwaruhusu wanawake kufanya kazi karibu na maeneo ya vita.

Maafisa katika makao makuu ya jeshi ya Pentagon wanasema mpango huo utatoa maelfu ya kazi kwa wanawake, ingawa kwa sasa hawataruhusiwa kushiriki vita moja kwa moja.

Hata hivyo makundi ya wakereketwa wa haki za wanawake yanasema hatua hiyo ni ndogo sana kuliko walivyotarajia.

Wanataka hatua zingine zaidi kuchukuliwa katika kuwahusisha wanawake katika vita moja kwa moja.