Mhubiri Abu Qatada aachiliwa kwa dhamana

Mhubiri wa kiislam mwenye siasa kali Abu Qatada ameachiliwa kwa dhamana kutoka gerezani nchini Uingereza baada ya kuzuiliwa kwa muda wa miaka sita unusu.

Amekuwa akizuiliwa huku serikali ya Uingereza ikijaribu kumpeleka Jordan ambapo anakabiliwa na tuhuma za ugaidi.

Hata hivyo kurejeshwa kwake Jordan kumezuiwa na mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya, kutokana na hofu kuwa huenda kesi yake isishugulikiwe kwa njia ya haki.

Serikali ya Uingereza inasema Abu Qatada ni tishio kwa usalama wa kitaifa.