Ndovu wengi wauawa nchini Cameroon

Ripoti mpya inasema wawindaji haramu wameua takriban ndovu 200 kaskazini mwa Cameroon, katika siku za hivi karibuni.

Shirika la kimataifa linaloshugulikia maslahi ya wanyama, linasema wapiganaji wa kigeni wanawinda ndovu hao ili wauze pembe kutafuta fedha, kufadhili machafuko nchini Sudan na Afrika ya Kati.

Shirika hilo linasema wapiganaji hao wamekuwa wakivuka mipaka ya eneo hilo kwa miaka mingi lakini kiwango hicho cha uwindaji haramu hakikutarajiwa.

Wanaharakati wa mazingira wanakadiria kuwa mwaka jana ndovu 3,000 waliuawa kinyume cha sheria barani Afrika.