Ugiriki:Mawaziri wakutana Brussels

Mawaziri wa fedha kutoka jumuiya ya ulaya wanakutana leo mjini Brussels kuamua kuhusu mkopo mpya kwa Ugiriki.

Katika makubaliano hayo Ugiriki itapewa mkopo wa zaidi ya dola Bilioni 170 mbali na kufutiliwa mbali kwa deni lake.

Makubaliano hayo yamegonga mwamba katika siku zilizotangulia kutokana na Ugiriki kutotimiza masharti iliyowekewa kabla ya kupewa mkopo huo.