Watu 20 wauawa Maiduguri

Wahudumu wa hospitali katika mji wa Maiduguri, nchini Nigeria, wanasema wamepokea takriban miili 20 ya watu waliokufa katika milipuko na mashambulio ya risasi kati ya wanajeshi na wanamgambo wa Boko Haram kwenye soko.

Vikosi vya usalama vimesema viliwaua wanamgambo wanane , lakini vikakanusha kuuawa kwa raia yeyote.

Mji wa Maiduguri ulioko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, umekuwa ukikumbwa na mashambulio ya mara kwa mara yanayofanywa na kundi la wanamgambo wa Kiislam la Boko Haram.