McCain ataka waasi kusaidiwa Syria

Seneta wa Marekani, John McCain ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa msaada kwa waasi wanaopinga serikali ya Syria.

Amesema Marekani inaweza kutoa misaada ya kimatibabu na kiufundi kwa vikosi vinavyopigana dhidi ya serikali ya rais Bashar Al Assad.

Aliongeza kuwa Marekani, haipaswi kuwapatia waasi silaha moja kwa moja, lakini kuna njia nyingine za kuingiza silaha ndani ya Syria ili kuwawezesha kupigana na wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo.

Bwana McCain, ambaye alikuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican katika uchaguzi wa mwaka 2008 , alikuwa akizungumza nchini Misri.