ICC kuchunguza ghasia za Ivory Coast

Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC iliyoko mjini The Heague imeongeza zaidi uchunguzi wake juu ya uhalifu wa kivita nchini Ivory Coast, kufuatia uchaguzi wa mwaka 2010 uliozua ghasia, ambapo Rais Laurent Bagbo aliyeshindwa alikataa kuachia madaraka.

Waendesha mashtaka katika mahakama hiyo ya ICC, pia watachunguza makosa ya uhalifu wa kivita na ukatili dhidi ya binadamu, yaliyofanywa kuanzia Septemba 2002 na kuendelea wakati liliposhindwa jaribio la mapinduzi dhidi ya rais laurent Bagbo.

Kwa pamoja waasi na vikosi vinavyounga mkono serikali wanashutumiwa kwa makosa ya uhalifu.