Miji China haifikii viwango hewa safi

Theluthi tatu ya miji yaChinaitashindwa kufikia kiwango kipya kinachotalikiwa cha hewa, afisa mwandamizi wa mazingira amesema.

Maelezo hayo kutoka kwa makamu wa waziri wa Ulinzi wa mazingira Wu Xiaoqing yamekuja siku mbili baada ya baraza la mawaziri kutangaza kupitia upya viwango vya hewa ambavyo vitaanza kutumika mwaka 2016.

Kiwango cha hewa nchiniChinakimeendelea kuwa kibaya licha ya kukua kwa uchumi kwa kasi.

Katika miezi ya karibuni watu wametaka kuwe na mabadiliko ya namna ya kufuatilia mitandao ya kudhibiti uchafuzi wa hali ya hewa.

Chini ya viwango hivi vipya vipimo vya ukanda wa ozoni na kiwango cha mkandamizo wake wa PM2.5 – kinafikia kiasi kidogo kuliko 2.5 kipimo cha micrometa ndani ya mzingo-kitafuatiliwa.