Mwanzilishi wa Biafra azikwa Nigeria

Maelfu ya watu kusini mashariki mwa Nigeria wamehudhuria mazishi ya kiongozi wa zamani wa vuguvugu la Biafra Chukwuemeka Odumegwu-Ojukwu.

Mwandishi wa BBC Fidelis Mbah, akiwa nyumbani kwa Kanali mjini Nnewi, alisema watu wenye mapenzi mema walipanga mistari mitaani na kupanda majengo marefu ili waweze kuona.

Kanali Ojukwu alikufa nchini Uingereza mwaka jana baada ya kuugua kwa muda mrefu akiwa na miaka 78.

Kujitangazia kwake uhuru waBiaframwaka 1967 kulizusha vita vya wenyewe kwa wenyewe na watu zaidi ya milioni moja walikufa.

Anabakia kuwa nguzo mtu maarufu katika siasa zaNigeria, akiwania Urais wa nchi hiyo mara mbili katika miaka ya 2000.