Wanariadha Uingereza watahadharishwa

Wanariadha nchini Uingereza wametahadharishwa dhidi ya kuamkuana kwa mikono wakati wa kipindi cha michezo ya Olmpiki nchini humo.

Daktari mkuu wa chama cha michezo ya olimpiki cha Uingereza, Ian McCurdie, aliwafahamisha wanariadha kwamba wasisalimiane kwa mikono ili kupunguza uwezo wa kuambukizwa maradhi yatakayowaathri kiasi cha kukosa kushiriki michezo hiyo.

Alisema kuwa ikiwa wachezaji hao watashurutishwa kusalimiana kwa mikono, na washindani wao lazima wanawe mikono baadaye.