Yatakiwa Sepp Blatter kuchunguzwa

Kamati ya wanasiasa barani Ulaya, imelitaka shirikisho la soka duniani FIFA, kuchunguza utaratibu uliotumika kumchagua tena rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter mwaka jana.

Kamati hiyo pia inataka kuchapishwa kwa stakabadhi kuhusu madai ya ufisadi dhidi ya bwana Blatter.

Aidha kamati hiyo inataka uchunguzi ufanywe kuhusu ikiwa yeyote hasa Blatter mwenyewe alitumia ushawishi wake kushinda uchaguzi huo, swala ambalo ni kinyume na maadili ya uchaguzi.

Imeitaka FIFA kuchunguza kashfa ambazo zimeiharibia sifa soka ya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni.