Anders Behring Breivik ashtakiwa

Mtu aliyekiri kufanya mauaji makubwa nchini Norway mwaka jana hatimaye ameshtakiwa rasmi kwa makosa ya kigaidi na mauaji ya makusudi.

Anders Behring Breivik, mfuasi wa siasa kali, anatarajiwa kufikishwa mahakamani mwezi ujao.

Mwezi Julai mwaka jana, Anders Behring Breivik, aliwaua watu tisa katika mashambulizi yake ya kiholela aliyoyafanya na mauaji ya wengine wanane katika shambulizi la bomu.

Viongozi wa mashtaka, wataitaka mahakama kuruhusu azuiliwe katika taasisi ya wagonjwa wa kiakili baada ya wataalamu kusema kuwa ana kichaa.