Wanajeshi waingereza wauawa Afghanistan

Wanajeshi sita wa wa uingereza wameuawa katika mlipuko uliotokea katika jimbo la Kandahar nchini Afghanistan.

Vifo hivi vinafikisha idadi ya wanajeshi wa Uingereza waliouawa kuwa zaidi ya mianne. Wanajeshi hao walikuwa wakishika doria wakati Gari lao la kivita lilipolipuliwa.

Hili ndio tukio la vifo vingi kwa wakati mmoja kukumba jeshi la Uingereza nchini Afghanistan tangu kudunguliwa kwa ndege ya kijasusi mwaka 2006 ambapo wanajeshi kumi na wanne waliopuawa.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza inasema wanajeshi hao hawajulikani waliko na hivyo inadhaniwa kuwa wamekufa..