Vifo vya mateka, Uingereza yalaumiwa

Rais wa Italia Giorgio Napolitano amelalamikia Uingereza baada ya operesheni ya kuwaokoa mateka wawili akiwemo mhandisi mwingereza na mwenzake wa Italia kutibuka.

Wawili hao waliuawa hapo jana na watu waliokuwa wamewakamata nchini Nigeria.

Amelezea kushangazwa kwake na hatua iliyochukuliwa na Uingereza bila kushauriana na upande wake, kabla ya kuanza operesheni ya kuwaokoa Christopher McManus na Franco Lamolinara.

Awali mwandishi wa BBC nchini Nigeria alielezea kuwepo na makabiliano makali yaliyochukua saa kadhaa ambapo baadaye aliona maiti wawili na wanajeshi wa Nigeria.

Serikali ya Uingereza imesema operesheni hiyo iliongozwa na kikosi chake maalum.