Uingereza yakana kuingilia utawala Kenya

Serikali ya Uingereza imekanusha madai ya mbunge wa Kenya kwamba inapanga njama za kumfungulia mashtaka ya uhalifu rais Mwai Kibaki katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.

Mbunge huyo wa Kenya Charles Kilonzo alisoma barua bungeni akidai imeandikwa na afisaa kutoka ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Uingereza.

Hata hivyo ubalozi wa Uingereza mjini Nairobi umesema tuhuma hizo ni kampeini ya kuharibu uhusiano kati ya Kenya na Uingereza na kuitaja barua hiyo kama isiyo ya kweli.

Raia wanne mashuhuri wa Kenya wanachunguzwa na mahakama ya ICC kutokana na machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2008.