Rais Hugo Chavez akamilisha matibabu

Rais Hugo Chavez wa Venezuela amesema atarejea nyumbani huko Caracas kabla ya mwisho wa juma hili baada ya matibabu zaidi ya saratani nchini cuba.

Katika mkutano na baadhi ya mawaziri wake waliomtembelea huko Havana, bwana chavez alisema kuwa anapata nafuu kufuatia upasuaji wa kuondoa sehemu iliyoathirika na saratani mwilini mwake.

Lakini alisema kuwa atahitaji kufanyiwa matibabu zaidi katika majuma yajayo.

Kiongozi huyo aliyegundulliwa kuwa na ugonjwa huo mwaka jana, ametangaza kuwa atawania tena urais katika uchaguzi wa Novemba.