Mageuzi ya haraka China

Waziri mkuu wa China , Wen Jia Bao, ametoa wito wa kufanyika kwa mageuzi zaidi ya kisiasa akisema yanahitajika haraka kwa ajili ya kulinda faida za kiuchumi za Uchina.

Kwa namna ya kipekee amesema mfumo wa uongozi wa chama na nchi vinahitaji mabadiliko.

Bwana Wen ameonya kuwa bila mageuzi , Uchina inakabiliwa na tisho la kurejea katika hatari ya kile alichotaja kuwa ni maafa ya mapinduzi ya kiutamaduni ya miaka ya 60.

Akizungumza katika kikao cha mwisho wa mwaka cha bunge, waziri mkuu huyo wa Uchina pia liomba msamaha kwa matatizo yaliyojitokeza wakati wa muongo mmoja wa utawala wake.