Mauaji karibu na Ikulu Somalia

Watu watatu wameuawa kwenye mlipuko wa bomu katika mji mkuu wa somalia mogadishu karibu na ikulu ya rais.

Msemaji wa jeshi la Muungano wa Afrika mjini humo, amesema kuwa mlipuko huo ulitokea karibu na makaazi rasmi ya spika wa bunge la nchi hiyo.

Eneo hilo liko karibu sana na eneo ambalo lina ulinzi mkali mjini Mogadishu

Wanamgambo wa Al Shabaab wametekeleza mashambulio kadhaa ya mabomu mjini humo tangu kufurushwa na wanajeshi wa serikali ya mpito kwa ushirikiano na wanajeshi hao wa Muungano wa Afrika mwaka uliopita.