Ethiopia yashambulia jeshi Eritrea

Serikali ya Ethiopia inasema imeshambulia kambi za kijeshi nchini Eritrea, ambazo inasema zilikuwa zinatumiwa kutoa silaha na mafunzo kwa wanamgambo.

Msemaji wa serikali, Shimeles Kemal, ameshutumu Eritrea kwa kutumia wanamgambo kushambulia Ethipia kwa niaba yake.

Alilaumu makundi hayo kwa kuwateka nyara na kuwaua watalii nchini Ethiopia mnamo mwezi Januari.

Nchi hizo mbili ziliwahi kupigania mpaka kati ya mwaka 1998 na 2000. Uhusiano kati ya nchi hizo ulizorota na imesalia kuwa hivyo hadi leo.