Maafisa wakuu Misri hatiani

Kiongozi mkuu wa mashtaka nchini Misri ameagiza kuwa watu sabini na watano, wakiwemo maafisa kadhaa wakuu waandamizi wa ulinzi, wafunguliwe mashtaka.

Maafisa hao wanahusishwa na ghasia zilizoibuka katika uwanja mmoja wa soka na kusababisha vifo vya zaidi ya watu sabini.

Ghasia hizo zilizotokea mjini Pitrer Februari zilitokea baada ya mechi kati ya El Masry na El Ahly ya Cairo.

Uchunguzi uliofanywa na kamati ya bunge imelaumu maafisa wa polisi kwa kutowajibika ili kuzuia ghasia kati ya mashabiki wa timu hizo mbili.

Maandamano kadhaa yalitokea kufuatia ghasia hizo huku maelfu ya raia wakishutumu baraza la utawala wa kijeshi kwa kushindwa kutoa ulinzi wa kutosha.