Mauritania kumkabidhi Al Senussi

Afisa wa juu katika serikali ya Libya amesema Mauritania imekubali kumkabidhi aliyekuwa mkuu wa ujasusi Abdullah Al-Senussi kwa maafisa wa Tripoli.

Naibu Waziri Mkuu Mustafa Abu Shagour, alitoa tangazo hilo baada ya kukutana na rais wa Mauritania Ould Abdel Aziz.

Hata hivyo maafisa wa Mauritania wamesema hakuna uamuzi ulioafikiwa kuhusu kumkabidhi afisaa huyo wa zamani.

Bw Senusi anayetajwa kuwa mwandani wa kiongozi wa Libya aliyetimuliwa madarakani Kanali Muammar Gaddafi, ametuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kibinadamu wakati wa maandamano ya kushinikiza mageuzi ya kidemokrasia mwaka jana.

Serikali ya Ufaransa inamtaka Al-Senussi kwa tuhuma za kuhusika na ulipuaji wa ndege ya abiria mwaka 1989.