Hawataki kukosolewa

Kundi la wataalamu linalochunguza visa vya udanganyifu na utumiaji wa madawa haramu miongoni mwa wanariadha katika michezo ya olimpiki, limeshutumiwa kwa kujaribu kuwanyamazisha wakosoaji wake.

Lawama hizo zimetolewa na mmoja wa wanasayansi wakuu wa kuchunguza madawa haramu Michael Ashenden, ambaye ametangaza kuwa anajiuzulu kutoka shirika hilo kwa jina Athlete Passport Unit.

Kundi hilo linaweza kuchunguza udanganyifu wa wanariadha kwa kupata mabadiliko kidogo katika damu au mkojo.

Inakisiwa kuwa uvumbuzi wa juu zaidi katika spoti.