Obama ana imani na mpango wa afya

Rais Obama amesema ana imani kuwa maafisa wasiopendelea mabadiliko ambao ndio wengi katika mahakama ya juu ya nchi hiyo hawatapinga sheria mpya ya afya.

Rais Obama amesema majaji hawapaswi kupinga mpango huo uliopitishwa na idadi kubwa ya wabunge wa baraza la Congress.

Waandishi wa habari wanasema iwapo mahakama itakosa kupitisha sheria hiyo,hatua hiyo itaathiri juhudi za Rais Obama katika kampeni za kuwania urais mwezi Novemba.

Uamuzi wa mahakama unatarajiwa mwezi Juni wakati kampeni za uchaguzi wa urais zitakuwa zimepamba moto.

Waandishi wa habari waasema sio kawaida kwa rais kuzungumzia uamuzi ambao haujafanywa na huenda ikawa ishara kuwa anajua sheria hiyo itapitishwa.