Serikali ya Syria haina uwezo tena

Aliyekuwa makamu wa rais wa Syria , Rifaat al-Assad, anasema anaamini hakuna uwezekano wa serikali ya nchi hiyo kuendelea kuwa mamlakani chini ya utawala wa Rais Bashar al-Assad.

Rifaat al-Assad, ambaye ni mjomba wake rais wa sasa amesema kiwango cha machafuko nchini syria , kiko juu sana na itakuwa vigumu kwa serikali kusalia mamlakani.

Rifaat al-Assad amekuwa akiishi uhamishoni katika mji mkuu wa Ufaransa Paris,tangu jaribio lake kuipindua serikali iliyokuwa ikiongozwa na nduguye kukosa kufaulu katika miaka ya themanini.