Ugiriki yasimamisha michezo yote

Shirikisho la mchezo wa riadha nchini Ugiriki linasema limesimamisha shughuli zote za kimichezo nchini humo kutokana na ukosefu wa fedha.

Halmashauri kuu ya Shirikisho hilo inayosimamia michezo imesema baada ya mkutano wa dharura ,kwamba watazingatia uamuzi huo pindi serikali itafikiria upya uamuzi wake wa kupunguza kwa kiwango kikubwa msaada wake wa fedha kwa michezo. .