Wanajeshi waondoka jeshini DRC

Mamia ya vikosi vya jeshi la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, wameondoka jeshini.

Wanajesi hao waasi, ni watiifu kwa aliyekuwa kiongozi wa waasi, Bosco Ntaganda, anayetakikana na mahakama ya jinai ya ICC kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Generali Ntaganda, aliingiza vikosi vyake katika jeshi la DRC mwaka 2009.

Kufuatia shinikizo kutoka kwa serikali ya Ubelgiji, ambayo wiki jana ilimtaka rais Joseph Kabila, kumkamata Ntaganda, ndio imekuwa sababu kuu ya wanajeshi hao kuondoka jeshini.

Msemaji wa jeshi la serikali, kanali, Sylvian Ekenge, alisema yeyote atakayepatikana na hatia ya kuhusika na kitendo chochote cha kuvunja sheria jeshini ataadhibiwa.