Seif al Islam hatakabidhiwa ICC

Serikali ya Libya imesisistiza kuwa Saif AL Islam, mwanaye kiongozi wa nchi hiyo aliyeuawa, Muammar Gaddafi, atashtakiwa nchini humo badala ya kupelekwa kwa mahakama ya kimataifa ICC.

Hapo jana Mahakama hiyo ya ICC iliitaka serikali ya Libya kufanya mipango ya kumkabidhi Saif Al Islam mjini the Hague. Saif Alikamatwa Novemba mwaka jana.

Serikali hiyo hata hivyo inasema kuwa mipango iko tayari kwa Seif kufunguliwa mashtaka lakini haijasema ni lini kesi hiyo itaanza kusikizwa.

Kundi la kijeshi kutoka mji wa Zintan ndilo linalomshikilia Saif akisubiri kesi yake.