Kofi Anaan ana matumaini na Syria

Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa na jumuiya ya nchi za kiarabu nchini Syria, Kofi Annan, ameelezea matumaini yake ya kusitishwa kwa vita nchini humo katika siku mbili zijazo.

Huu ndio muda uliosalia kabla ya kukamilika kwa makataa aliyotoa kwa nchi hiyo kukomesha vita ifikapo Jumanee wiki ijayo.

Msemaji wa bwana Annan, amesema kuwa wanajeshi wa Syria mwanzo wanastahili kuondoka kutoka maeneo ya mijini kwanza, na kisha kusitisha mapigano mara moja kwa pande zote mbili.

Makataa hiyo ni sehemu ya mpango wa amani uliotolewa na Koffi Anaan, ambao rais wa Syria Bashar al-Assad, ameukubali.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Alain Juppe, amesema kuwa anaamini rais Asaad anahadaa jami ya kimataifa na kuwa hana matumaini mpango huo utafanikiwa.