Khumbo Kachali awa Makamu Rais Malawi

Rais mpya wa Malawi Bibi Joyce Banda amemteua makamu wake wa Rais, Khumbo Kachali.

Bw Khumbo anashika nafasi hiyo akiwa ni mbunge wa Mzimba Kusini kutoka chama cha People's (PP)

Bibi Banda anaendelea kutikisa serikali kwa kuteua viongozi wapya baada ya kushika wadhifa huo siku ya Jumamosi.

Rais mpya wa Malawi Joyce Banda amekuwa akitumia vyema madaraka yake tangu ashike wadhifa huo baada ya kifo cha mtangulizi wake Bingu wa Mutharika.

Bibi Banda - ambaye ametokea chama cha upinzani amewafuta kazi watu muhimu waliokuwa katika utawala wa Mutharika akiwemo mkuu wa polisi Peter Mukhito.