Wanawake Uzbekistan watolewa vizazi

Uchunguzi wa BBC umegundua kile kinachoonekana kama mpango wa siri wa kuua uwezo wa wanawake kuzaa nchini Uzbekistan.

Mwandishi wa BBC Asia ya Kati amezungumza na wanawake ambao wamefanywa wagumba bila ya ridhaa yao au bila kujua.

Madaktari wanasema wizara ya afya ya Uz-bek imetoa amri ya kuhudhuria mpango huo wa kuwahasi kila mwezi madai ambayo serikali imeyakanusha.

Sehemu kubwa ya via vyao vya uzazi zimefungwa na baadhi ya tumbo la uzazi limeondolewa baada ya kujifungua mtoto wa pili au wa tatu.

Wanawake waliohojiwa na BBC walisema waume zao waliwatelekeza waliogundua hali hizo.