EU yalaani Argentina kwa kutwaa YPF

Muungano wa Ulaya unatafakari hatua gani nyingine za kuchukua dhidi ya Argentina kufuatia mpango wa kutaifisha kampuni ya mafuta inayomilikiwa na Hispania YPF.

Tangazo la Rais wa Argentina Cristina linafuatia taharuki ya miezi ya karibuni kati yake na Uingereza dhidi ya umiliki wa kisiwa cha Falkland.

Kamishina wa masuala ya nje wa EU Catherine Ashton, amesema Muungano huo unaunga mkono Hispania kupinga hatua hiyo.

Waziri Mkuu wa Hispania Mariano Rajoy amesema Argentina haina haki ya kutaifisha kampuni hiyo akisema itaathiri pande zote.

Rais Fernandez amepuzilia vitisho vyovyote akisema amefanya maamuzi hayo kwa maslahi ya raia wa Argentina.