IMF yasema uchumi wa dunia shwari

Shirika la Fedha duniani limeelezea kuwepo dalili za kuimarika uchumi wa dunia japo kwa pole.

Katika tathmini yake IMF imetaja bei ya mafuta na matatizo ya madeni yanayokumba kanda ya Euro kama tisho kubwa.

Pia imeonya uwezekano wa baadhi ya nchi kujiondoa kanda ya Euro na kusema endapo hili litatokea, litasababisha athari kubwa kwa uchumi wa dunia ,kuliko ilivyokuwa baada ya kuporomoka kwa benki ya uwekezaji ya Lehman Brothers mwaka 2008.

IMF inasema ukuaji wa sasa haukutarajiwa katika miezi ya karibuni na kwamba ni ishara za matumaini.