Umoja wa mataifa wakemea S Kusini

Umoja wa mataifa umelaani kitendo cha Sudan kusini kuteka machimbo ya mafuta ya Heglig katika mpaka wanaozozania na Sudan.

Katibu mkuu Ban Ki-moon amesema kuwa kitendo hicho ni uvunjaji wa sheria na kuitaka nchi hiyo kuondoa vikosi vyake mara moja.

Bwana Ban pia amekosoa serikali ya Khartoum na kuimauru kusitisha mashambulizi ya wanajeshi wake katika eneo hilo linalozozaniwa na nchi hizo.

Aliongeza kuwa pande zote mbili sharti ziache kuunga mkono majeshi dhidi ya upande mwingine.