Syria yadaiwa kuagiza silaha

Serikali ya Uturuki, inasaka meli moja ya mizigo inayoaminika kusheheni silaha zilizokuwa zinasafirishwa nchini Syria kutoka Iran.

Meli hiyo, Atlantic Cruiser, imetia nanga katika bandari ya Uturuki, ya Iskenderun katika bahari ya Meditarenia.

Wanaharakati nchini Syria, wametahadharisha kuwa nchi hiyo itakuwa inakiuka marufuku iliyowekewa na nchi za magharibi ya kutonunua silaha kutoka nje mwaka mmoja uliopita.

Wamiliki wa meli hiyo ambao ni wajerumani kwa ushirikiano na kampuni moja ya Ukrain, wamekana kuwa meli hiyo imesheheni zana za kivita.

Wanaharakati wanadai kua meli hiyuo ilikuwa ma silaha wakti ilipotia nanga nchini Djibouti.