Kesi ya wahanarakati kuanza tena

Mahakama ya Bahrain imeagiza kurejelewa kesi ya mwanaharakati wa kisasa ambaye amesusia chakula wakati akiwa kizuizini.

Abdul-Hadi al-Khawaja pamoja na wanaharakati wengine 20 walihukumiwa jela na mahakama ya kijeshi mwaka jawna.

Kesi dhidi yao sasa itasikilizwa mbele ya mahakama ya kiraia.Mkewe amesema maafisa wa Buhrain wanatumia kesi hii kama njama ya kujaribu kusafisha sifa ya nchi.

Amesema hakuna tofauti ya mfumo wa sheria licha ya kesi ya mumewe kuhamishiwa katika mahakama ya kiraia.