Aung San Suu Kyi kuapishwa bungeni

Kiongozi anayetetea sera za kidemokrasia nchini Burma amesema atakubalia kuapishwa pamoja na wabunge wa chama chake na hivyo kumaliza mzozo wa kisiasa uliokuwepo.

Aung San Suu Kyi amesema uwamuzi wake umetokana na matakwa ya raia ambao wanamtaka kuingia bungeni.

Chama chake cha NLD kilisusia kuapishwa kutokana na maandishi kwenye kiapo hicho.

Kiapo kilichozua utata kinawataka wabunge kuapa kulinda katiba ambayo iliandikwa chini ya utawala wa kijeshi. Wabunge wapya wanatarajiwa kuanza vikao vyao wiki hii.