Watu kadhaa wauawa Idlib

Watu kadhaa wameuawa kufuatia mlipuko wa bomu katika mji wa kaskazini-magharibi wa Idlib nchini Syria, wanaharakati pamoja na kituo cha televisheni cha taifa wamesema.

Taarifa kutoka kituo cha televisheni zinasema kuwa milipuko miwili iliwaua watu wanane, huku kundi la kutetea haki za binadamu la Syria likisema kuwa zaidi ya watu 20 wameuawa katika shambulio lililolenga vikosi vya usalama.

Umoja wa Mataifa kwa sasa unatuma wachunguzi wake katika nchi hiyo ili kushughulikia mchakato wa amani.

Wachunguzi thelathini watafika katika eneo hilo hivi karibuni lakini Umoja wa Mataifa unasema utahitaji wachunguzi zaidi.