Kadinal Sean Brady asema hatajiuzulu

Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki nchini Ireland, amesema hatajiuzulu kufuatia madai kuwa hakuwajibika ipasavyo, kuwalinda watoto kadhaa wanaodaiwa kudhulumiwa na makasisi wa kanisa hilo.

Kadinali Sean Brady, amesema madai yaliyojitokeza katika kipindi kimoja cha Idhaa ya BBC, iliangazia pakubwa majukumu yake katika uchunguzi dhidi ya padre Brendan Smyth miaka ya sabini.

Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyomba vya habari, Kadinali Brady, ameelezea majukumu yake katika uchunguzi huo na kusema kwamba anahisi kuwa alisalitiwa.

Amesema watu ambao walikuwa na uwezo wa kumzuia padre Smyth kutekeleza uovu huo hawakuwajibika.

Lakini amekiri kuwa alikuwa mmoja wa wale ambao hawakusema lolote kuhusu suala hilo na hivyo kutosaidia katika uchunguzi wa sakata hiyo.