Clinton ataka ushirikiano zaidi na China

Mawaziri wawili wa ngazi ya juu katika serikali ya Marekani, Hillary Clinton na Timothy Geithner, wameanza mazungumzo mjini Beijing.

Katika hotuba ya wazi , Bi Clinton amesema Uchina na Marekani haziwezi kumaliza matatizo yote ya dunia, lakini kuna hofu kwamba nchi hizo mbili haziwezi kuafikia malengo yao pasipo ushirikiano baina yao.

Rais wa china Hu Jintao, amesema nchi hizo mbili zinapasa kuheshimiana hata zinapotofautiana.

Mazungumzo ya awali yaligubikwa na tukio la mwanasiasa wa upinzani wa Uchina Chen Guang-cheng, aliyepata hifadhi kwenye ubalozi wa Marekani mjini Beijing baada ya kutoroka kifungo cha nyumbani.

Mwanaharakati huyo kwa sasa ameondoka kwenye ubalozi huo wa Marekani kwa ajili ya usalama wa familia yake , lakini anaripotiwa kuwa anataka kuondoka Uchina.