Korea Kaskazini yawekewa vikwazo na UN

Makampuni matatu ya taifa nchini Korea Kaskazini yamewekewa vikwazo na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Baraza hilo limezitaka nchi zote kuzuia mali zote za kampuni hizo tatu, ili kujibu hatua ya Korea Kaskazini ya kufanya jaribio la roketi lililoshindwa.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, amesema viwanda hivyo vilihuzika katika mipango ya taifa ya makombora ya masafa marefu na nuklia.

Marekani, muungano wa ulaya, Korea Kusini na Japan, walitaka mashirika arobaini ya Korea Kaskazini na watu binafsi kujumuishwa katika orodha hiyo ya vikwazo.

Serikali ya Korea Kaskazini halijasema lolote kufuatia wito huo wa baraza la usalama na Umoja wa Mataifa.